Nategemea barua hii itakukuta salama. Mimi ni msichana wa
miaka 23. Nilifiwa na wazazi wangu wakati nikiwa na miaka minane. Bibi yangu
alishindwa kunilipia shule hivyo nikawa nyumbani tu, bahati nzuri mvulana mmoja
kijijini kwetu akanambia atanisaidia, wakati huo alikuwa anauza machungwa
barabarani. Kweli alianza kunilipia shule, miaka yote, hatimae hata yeye
akabadili kazi akaanza kuendesha daladala, na ameendelea kunilipia mpaka sasa
niko chuo kikuu. Namshukuru Mungu kwa kunikutanisha na malaika kama huyu sijui
siku hizi ningekuwa wapi
Tatizo langu ni kuwa anataka kunioa nikimaliza chuo, na mimi kwa kweli nashindwa kumwambia kuwa itakuwa vigumu kwa kuwa yeye siyo 'type' yangu. Hebu fikiria mimi ni graduate halafu naolewa na dreva wa daladala, ni wazi kuwa si type yangu. Ninachoomba ni busara zako ntamwambiaje bila kumuumiza, kuwa haiwezekanai mimi nikaolewa na yeye?

No comments:
Post a Comment