Ufahamu wa
uwezo wa kushika mimba , (FA) unarejelea jumla ya mambo yanayotumiwa kuamua
wakati mwanamke anapoweza kushika mimba na asipoweza kushika mimba katika
mzunguko wa hedhi. Mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba zinaweza kutumiwa
ili kuzuia
mimba, na kutunga
mimba, au kama njia ya kusimamia afya ya uzazi wa mwanamke.
Mbinu za
kubaini siku ambazo mwanamke hawezi kupata mimba zinajulikana tangu zamani,
lakini ujuzi wa kisayansi uliopatikana katika karne ya iliyopita imeongezeka
sana usahihi wa mbinu hizo. Kutoka 1930-1980, utafiti wote na ukuzaji wa uelewa
wa masuala ya uzazi ulifanywa na wanaohusishwa na Kanisa Katoliki la Kirumi.
Mashirika ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba yanaendelea kudhibitiwa na
Katoliki, lakini baadhi ya mashirika ya kawaida sasa yapo.
Mifumo ya
ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutegemea uchunguzi wa mabadiliko ya ishara
moja au zaidi ya kimsingi yanayoashiria uwezekano wa kutunga mimba (joto la
kimsingi la mwili, kamasi ya seviksi, na mkao wa seviksi), kufuatilia mzunguko
wote wa hedhi na kubaini wakati ambapo inawezekana kushika mimba kulingana na
habari hii, au zote mbili. Ishara nyingine pia zinaweza kuzingatiwa: hizi ni
pamoja na ulaini wa matiti na miteliskimazi (uchungu wakati yai
linapoachiliowa), uchunguzi wa vifaa vya kukagua mkojo vinavyojulikana kama
vifaa vya kubashiri mayai, ufupisho Kiingereza (OPKs), na uchunguzi wa
kihadubini wa mate au ugiligili wa seviksi. Pia njia ya kufuatilia uwezo wa
kushika mimba kwa tarakilishi unapatikana.
Istilahi
Mbinu
zinazotegemea dalili zinahusisha kufuatilia ishara moja au zaidi kati ya ishara
tatu za kimsingi za kuweza kutunga mimba - joto la kimsingi la mwili, kamasi ya
seviksi, na mkao wa seviksi.[1] Mifumo
zinazotegemea kamasi ya seviksi ni pamoja na Mtindo wa Billing wa Kutambua Yai,
Mtindo wa Creighton, na Mbinu ya Siku Mbili. Mbinu za dalili za joto la mwili
hujumuisha uchunguzi wa joto la kimsingi la mwili (BBT), kamasi ya seviksi, na
wakati mwingine mkao wa seviksi. Mbinu za kalenda hutegemea kufuatilia mzunguko
wa hedhi ya mwanamke na urefu wa mzunguko wake kutambua anapoweza kutunga
mimba. Mbinu bora inayojulikana kati ya hizi ni Mbinu ya Siku Wastani ambayo
ndiyo msingi wa mbinu ya kutazamwa kutumia kifaa kiitwacho CycleBeads. Mbinu ya
Urari-Kalenda pia huzingatiwa njia ya kutegemea kalenda, ingawa haijafanuliwa
vizuri na ina maana tofauti kwa watu tofauti.
Mifumo za
ufahamu wa uzazi zinaweza kutatwa kuwa Mbinu za Uzazi zinazoegemea Ufahamu(mbinu
za MUUFA ), [2] istilahi Mbinu
za Uelewa wa Uzazi (MUU) inahusu hasa mfumo uliofundisha na Toni Weschler. Neno
"mbinu asili ya uzazi wa mpango" (NFP) wakati mwingine hutumiwa
kutaja matumizi ya mbinu yoyote ya Ufahamu wa Uzazi FA. Hata hivyo, NFP
kimahsusi inahusu mbinu zilizoidhinishwa na Kanisa Katoliki: kutoweza
kutungisha wakati wa kunyonyesha, na kutoshiriki ngono katika kipindi ambapo
kuna uwezekano wa kupata mimba. Mbinu ya FA inaweza kutumika kwa watumiaji NFP
kutambua nyakati hizi rutuba.
Wanawake
wanaonyonyesha na wangependelea kuzuia mimba wanaweza kutumia mbinu ya
kukatizwa kwa hedhi wakati wa kunyonyesha (LAM). LAM ni tofauti na ufahamu wa
uzazi, lakini kwa sababu haihusishi vifaa au kemikali, mara nyingi huwasilishwa
pamoja na Ufahamu wa Uzazi FA kama njia ya kudhibiti uzazi.
Historia
Ukuaji wa mbinu zinazotegemea kalenda
Makala kuu ya: Calendar-based
methods#History
Haijulikani
hasa ni wakati gani iligunduiwa kwa mara ya kwanza kuwa wanawake wana vipindi
vya kutunga mimba na visivyo vya kutunga mimba vinavyoweza kutabirika. Mt.
Agustino aliandika
kuhusu uepukaji ngono ili kuzuia mimba katika mwaka wa 388 ( Wamanicheani
walijaribu kutumia njia hii ili kubakia bila watoto, na Agustino akashutumu
matumizi yao ya kuacha kushiriki ngono kwa kipindi fulani).[3] Kitabu kimoja
kinasema kwamba kuacha kushiriki ngono kwa muda kulipendekezwa na "
watu wachache wasio wa kidini tangu katikati ya karne ya kumi na tisa,"
[4] lakini
ushawishi mkuu katika karne ya ishirini uliohamasisha mbinu za ufahamu wa uwezo
wa kushika mimba ulitoka katika Kanisa Katoliki.
Mnamo 1905
Theodoor Hendrik van de Velde, mwanajinakolojia wa Kiholanzi, alionyesha kuwa
wanawake hutoa yai mara moja tu katika mzunguko wa hedhi.[5] Mnamo 1920,
Kyusaku Ogino, mwanajinakolojia wa Kijapani, na Hermann Knaus, kutoka Austria,
wakifanya kazi mbalimbali waligundua kwamba yai hutokea yapata siku kumi na nne
kabla ya kipindi cha hedhi inayofuata.[6] Ogino alitumia ugunduzi
wake kutengeneza mfumo wa kutumiwa katika kuwasaidia wanawake kupata mimba kwa
muda wa ngono na kufikia mimba. Mnamo 1930, John Smulders, daktari wa Mkatoliki
kutoka Uholanzi, alitumia ugunduzi huu kuunda mbinu ya kuepuka mimba.
Smulders alichapisha kazi yake kwa chama cha matabibu wa Kikatoliki cha
Uholanzi, na huu ulikuwa mfumo wa kwanza rasmi wa kuacha kujamiiana kwa kipindi
fulani - mbinu ya urari.[6]
Uanzilishi wa mbinu za dalili za joto na kamasi ya mlango
wa uzazi
Katika miaka ya
1930, Rev. Wilhelm Hillebrand, padri wa Kikatoliki nchini Ujerumani, alibuni
mfumo wa kuzuia mimba kutegemea joto la kimsingi la mwili.[7] Mbinu hii ya
joto ilipatikana kuwa na ufanisi zaidi katika kuwasaidia wanawake kuzuia mimba
kuliko mbinu ya kutegemea kalenda. Katika miongo michache iliyofuata, mifumo
hii miwili ikawa inatumika sana miongoni mwa wanawake Wakatoliki. Hotuba mbili
zilizotolewa na Papa
Pius XII mnamo 1951
zilitoa kielelezo cha juu cha kutambuliwa kwa mbiu hizi na Kanisa Katoliki-kwa
mume na mke waliotaka kuzuia mimba.[4][8] Katika mwanzo
wa miaka ya 1950, Dkt. John Billings aligundua uhusiano kati ya kamasi ya
mlango wa uzazi na uwezekano wa kutunga mimba alipokuwa akiifanyia kazi katika
Shirika la Kikatoliki la Usatawi wa Kijamii mjini Melbourne. Dkt. Billings na
madaktari wengine kadhaa walitafiti ishara hii kwa miaka kadhaa, na kufikia
mwishoni mwa miaka ya 1960 walikuwa wakifanya majaribio ya kkimatibabu na
kuanzisha vituo vya kufundisha duniani kote.[9]
Mashirika ya kwanza ya ufundishaji yaliyozingatia dalili
Japo awali Dkt.
Billings alifundisha dalili za joto na kamasi, walipata tatizo katika kufundisha
ishara za joto kwa idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika katika nchi
zinazoendelea. Katika miaka ya 1970 walibadilisha mbinu hiyo ili kutegemea
kamasi tu.[7] Jumuiya ya
kimataifa iliyoanzishwa na Dkt. Billings sasa inajulikana kama Shirika la
Watumiaji Mbinu ya Billings Duniani (WOOMB).
Shirika la
kwanza kufundisha mbinu za dalili na joto lilianzishwa mwaka 1971. John na
Sheila Kippley, waumini wa kawaida Wakatoliki, walijiunga na Dkt. Konald Prem
katika kufundisha mbinu ya kutazama iliyotegemea dalili zote tatu: joto,
kamasi, na pia mkao wa mlango wa uzazi. Shirika lao sasa linaitwa Shirika la
Wanandoa kwa Wanandoa la Kimataifa (Couple to Couple League International).[7] Muongo
uliofuata ulishuhudia kuanzishwa kwa mashirika mengine ya Kikatolikiambayo sasa
ni makubwa - Family of the Americans (1977), mafundisho ya mbinu za Billings,[10] na Taasisi ya
Papa Paulo VI (1985), inayofundisha mbinu ya kamasi pekee iitwayo Creighton
Model.[11]
Hadi miaka ya
1980, habari kuhusu ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ulipatikana tu kutoka
katika vyanzo vya Kikatoliki.[12] Shirika la
kwanza lisilo la kidini la mafundisho ya uzazi lilikuwa Kituo cha Uelewa wa
Uzazi cha New York, lililoanzishwa mwaka 1981.[13] Toni Weschler
alianza kufundisha manamo 1982 na kuchapishwa kitabu kilichouza sana cha Taking
Charge of Your Fertility katika mwaka wa 1995.[14] Justisse
ilianzishwa mwaka 1987 Edmonton, Kanada.[15] Mashirika haya
yote yasiyo ya kidini yanafundisha mbinu za dalili na joto. Ingawa mashirika ya
kikatoliki ni makubwa sana kuliko mashirika ya kiharakati yasiyo ya kidni
yanayoshughulikia uzazi, walimu wasiyo wa kujitegemea wa kidini wameongezeka
zaidi katika miaka ya 1990 na 2000.
Ustawishaji unaoendelea
Ustawi wa mbinu
za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaoendelea. Mwishoni mwa miaka ya 1990,
Taasisi ya Afya ya Uzazi katika Chuo Kikuu cha Georgetown ilianzisha mbinu
mbili mpya.[16][17] Mbinu ya Siku
Mbili, Mfumo wa kamasi tu, na CycleBeads, ni kibadala cha mbinu ya Mbinu ya
Urari, zimeundwa ili kuwa na ufanisi mkubwa na rahisi katika kufundisha,
kujifunza, na matumizi.
Ishara za uwezo wa kushika mimba
Mizunguko
nyingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kushika
(muda wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha yai), siku ambazo mimba inaweza
kutungika, na kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi
kutungika ( muda wa kutoshika mimba wa baada ya yai kudondoshwa). Siku ya
kwanza ya kuvuja damu nyekundu inahesabiwa kuwa siku ya kwanza ya mzunguko wa
hedhi. Mifumo mbalimbali ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba huhesabu kipindi
ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba kwa njia tofauti kidogo, kutumia ishara
za kimsingi za uwezekano wa kutunga mimba, historia ya mzunguko, au zote mbili.
Ishara za msingi
Ishara tatu za
msingi za uwezekano wa kushika mimba ni joto msingi la mwili (BBT), kamasi
ya seviksi, na mkao wa seviksi. Mwanamke anayetumia dalili msingi za
uwezo wa kutunga mimba anaweza kuchagua kutumia ishara moja, ishara mbili, au,
zote tatu.
Joto la msingi
la mwili ni joto la
mwili wa mtu wa linalochukuliwa wakati wa kwanza anapoamka asubuhi (au baada ya
usingizi wao wa muda mrefu wa siku). Miongoni mwa wanawake, kudondoshwa yai
husababisha kupanda kwa BBT kwa kati ya 0.3 na 0.9 ° C (0.5 na 1.6 ° F) ambayo
hubakia hivyo katika kipindi chote hadi wakati wa hedhi ijayo. Mabadiliko haya
ya joto yanaweza kutumika kubaini mwanzo wa kipindi cha kutotunga kabla ya
kudodosha yai.
Kamasi ya
seviksi
Kuonekana kwa kamasi
ya seviksi na mwasho wa uke ni ishara zinazoelezwa kwa pamoja kama njia
mbili za kubaini ishara hiyo. Kamasi ya seviksi huzalishwa na seviksi, ambayo
hutenganisha uterasi na mfereji wa uke. Kamasi ya seviksi yenye uwezo wa
kushika mimba hukuza maisha ya manii kwa kupunguza uasidi wa uke, na pia
husaidia kuongoza manii kupitia seviksi kuelekea ndani ya uterasi. Uzalishaji
wa kamasi ya seviksi yenye rutuba husababishwa na homoni moja (istrojeni)
ambayo pia huandaa mwili wa mwanamke kwa udondoshwaji wa yai. Kwa kuangalia
kamasi yake ya seviksi, na kuzingatia hisia ya jinsi inavyopita ukeni, mwanamke
anaweza kubaini wakati mwili wake unapojiandaa kudondosha yai, na pia wakati
ambapo udondoshwaji wa yai umepita. Wakati yai limedondoshwa, uzalishwaji wa
istrojeni hupungua na projesteroni huanza kuongezeka. Kupanda kwa kiwango cha
projesteroni husababisha mabadiliko katika wingi na hali ya kamasi
inayopatikana katika uke.[18]
Seviksi hubadilisha
mkao kutokana na homoni sawa inayosababisha kutolewa kwa kamasi ya seviksi
kukauka. Wakati mwanamke yuko katika awamu ya kutoshika mimba ya mzunguko wa
hedhi, seviksi hushuka chini katika mfereji wa uke, ikiguswa huwa ngumu (kama
ncha ya pua ya mtu), na, upenyu - kipenyo kinachoelekea katika seviksi -
itakuwa kidogo ikilinganishwa na wakati mwingine, au 'funge'. Jinsi mwanamke
anavyoongezeka kuwa na uwezo wa kushika mimba ndivyo seviksi kinavyopanda juu
ya mfereji wa uke, ni laini ukiguswa (laini kama mdomo wa mtu), na upenyu
utakuwa wazi zaidi. Baada ya kudondoshwa kwa yai, seviksi itarejea katika mkao
wake wa wakati ambapo si wa kushika mimba.
Historia ya mzunguko
Mifumo
inayotegemea kalenda hubainisha uwezekano wa kutopata mimba wa kabla na baada
ya kudondosha yai kulingana na historia ya mzunguko. Yanapotumia kuzuia mimba,
mifumo hii ina umadhubuti wa juu ukilinganishwa na mifumo inayotegemea dalili,
hata hivyo umadhubuti wake ni wa chini ukilinganishwa na mbinu zuizi kama vile
kiwambo na vizibo vya seviksi
Mbinu
zinazotegemea kamasi na joto la mwili kubaini uwezo wa kutunga mimba
zinapotumiwa kuepuka mimba, hudhihirisha matokeo katika matumizi ya chini sana
mimba viwango-kamilifu.[19] Hata hivyo,
mifumo ya kamasi na joto la mwili huwa na upungufu fulani katika kubaini uwezo
wa kutotunga mimba kabla ya kudondosha yai. Rekodi ya joto la mwili pekee
haitoi mwongozo wa uwezekano wa kutunga au kutotunga mimba kabla ya yai
kudondoshwa. Kubaini uwezekano wa kutoshika mimba kunaweza kufanywa kwa
kuchunguza kamasi ya seviksi; hata hivyo, hii hushuhudia matokeo yenye kiwango
cha chini cha ufanisi zaidi kuliko ile inayoshuhudiwa katika kipindi cha uwezo
wa kutokutungisha baada ya kudondosha yai.[20] Kutegemea
uchunguzi wa kamasi pekee pia ina maana kwamba kufanya ngono bila kinga
hairuhusiwi wakati wa hedhi, kwa sababu kamasi yoyote haitakuwa dhahiri.[21]
Matumizi ya
sheria fulani za kalenda kuamua urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba
kabla ya yai kudondoshwa huruhusu siku chache za ngono zembe katika siku za
kwanza za mzunguko wa hedhi huku kukiwa na kiwango cha chini sana cha uwezekano
wa kupata mimba.[22] Kwa kutumia
mbinu ya kamasi pekee, kuna uwezekano wa kutambua kimakosa kipindi cha katikati
ya mzunguko wa hedhi au kutoka damu katika mzunguko wa hedhi ambapo yai
halikudondoshwa. Kuweka chati sahihi ya Joto la Kimsingi la Mwili huwezesha
utambuzi sahihi wa hedhi, wakati ambapo sheria za kalenda zinazoshughulika na
kipindi kabla ya kudondosha yai zinaweza kutumiwa.[23] Katika mifumo
ya joto pekee, sheria ya kalenda inaweza kutegemewa pekee kuamua uwezekano wa
kutoshika mimba kabla ya kudondosha yai. Katika mifumo ya joto na ishara,
sheria ya kalenda huthibitishwa kwa rekodi za kamasi: uchunguzi wa kamasi ya
seviksi unaoashiria uwezo wa kupata mimba unapewa kipaumbele kuliko mbinu
yoyote ya kalenda ya kubainisha uwezo wa kushika mimba.[22]
Sheria za
kalenda zinaweza kuweka idadi mahsusi ya siku, inayobainisha kwamba (kulingana
na urefu wa mizunguzo iliyopita ya hedhi) siku tatu hadi sita za kwanza katika
kila mzunguko wa hedhi huchukuliwa kuwa isiyo na uwezo wa kupata mimba.[24] Au, sheria ya
kalenda inaweza kuhitaji hesabu, kwa mfano lazima iwe kwamba urefu wa kipindi
kabla ya kudondosha yai ni sawa na urefu wa muda mfupi zaidi sana wa mzunguko
wa hedhi ukiondoa siku ishirini na moja.[25] Badala ya
kufungiwa katika urefu wa mzunguko, sheria ya kalenda inaweza kubuniwa kutokana
na siku ya mzunguko ambapo mwanamke ameshuhudia mabadiliko katika joto la
mwili. Mfumo mmoja unasema urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba kabla ya
kudondosha yai unalingana na siku ya kwanza ambapo mwanamke aliposhuhudia kupanda
joto la mwili ondoa siku saba.[26]
Ishara andamizi
Wanawake wengi
huhisi ishara andamizi za uzazi zinazohusiana na awamu fulani ya mzunguko wa
hedhi. Mifano ni pamoja na maumivu ya tumbo na uzito, maumivu ya mgongo, ulaini
wa matiti na miteliskmazi (maumivu ya kudondosha yai).
Mbinu nyinginezo
Vifaa vya
kubashiri udondoshwaji wa yai (OPKs) inaweza kuchunguza udondoshwaji
unaotarajiwa kutegemea wingi wa homoni ya kuandaa ukuta wa chupa ya kizazi,
ufupisho wa Kiingereza (LH) katika mkojo na mwanamke. Ubashiri wa undondoshaji
wa kufana, hufuatiwa na udondoshaji ndani ya saa 12-36.
Uchunguzi
hadubini wa mate, ukifanyika kwa usahihi, unaweza kugundua vijidutu maalum
katika mate ambavyo hutangulia udondoshwaji wa yai. Vijidutu hivyo kwa kawaida
huonekana siku tatu kabla ya udondoshwaji yai, na kuendelea mpaka udondoshaji
utokee. Katika kipindi hiki, vijidutu hivi hutokea katika kamasi ya seviksi
pamoja na mate.
Vichunguza
uzazi vinapatikana kwa majina mbalimbali ta kibiashara. Vichunguzi hivi
vinaweza kutumia mifumo Joto la Kimsingi la Mwili BBT pekee, vinaweza
kuchanganua vitepe vya kupima mkojo, au vinaweza kuchunguza ukinzani meme wa
mate na ugiligili wa uke.
Faida na upungufu
Ufahamu wa
uwezo wa kushika mimba una kiwango fulani cha sifa bainifu:
- Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika kudhibiti afya ya uzazi. Mabadiliko katika mzunguko wa hedhi yanaweza kumtahadharisha mtumiaji kuhusu kujitokeza kwa matatizo ya kiginakolojia. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba pia unaweza kutumika kusaidia katika kuagua matatizo yanayojulikana ya kijinakolojia kama vile kutoweza kushika mimba.
- Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ni uwanda mpana: unaweza kutumika kuzuia mimba au kusaidia katika kutunga mimba.
- Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumiwa na wanawake wote katika kipindi chote cha uzazi, bila kujali ikiwa anakaribia kumaliza kuzaa, ananyonyesha, au anapata mzunguko wa hedhi usio wa kawaida kwa sababu zingine.
- Matumizi ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi mwili wa mwanamke unavyofanya kazi, na unaweza kuwaruhusu wanawake kuwa na udhibiti mkubwa wa uzazi wao wenyewe.
- Aina fulani ya mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba zinazotegemea dalili ya uzazi zinahitaji uchunguzi au kugusa kamasi ya seviksi, matendo ambayo baadhi ya wanawake hawafurahii. Baadhi ya wahudumu wanapendelea kutumia neno "majimaji ya seviksi" badala ya kamasi ya seviksi, katika juhudi ya kuwafanya wanawake kama hao kuhisi huru kidogo.
- Baadhi ya dawa, kama vile ya kupunguza kupaliwa mapafuni, yanaweza kubadili kamasi ya kizazi. Kwa wanawake wanaotumia dawa hizi, ishara ya kamasi huenda isionyeshe kisahihi uwezo wa kutunga mimba .[27]
- Baadhi ya mbinu zinazotegemea dalili huhitaji ufuatiliaji wa joto la kimsingi ya mwili. Kwa sababu usingizi usiokuwa na utaratibu unaweza kuvuruga usahihi wa joto la kimsingi la mwili, wafanyakazi wa kubadilisha zamu na walio na watoto wadogo sana, kwa mfano, huenda wasiweze kutumia mbinu hizo.[27]
Kama njia ya kupanga uzazi
Kwa kuhakikisha
kuwa ngono bila kinga inafanyika katika sehemu ambapo mimba haiwezi kushikika
katika mzunguko wa hedhi, mwanamke na mpenzi wake wanaweza kuzuia mimba. Wakati
ambapo mimba inaweza kushikwa katika mzunguko wa hedhi, wanandoa wanaweza
kutumia mbinu za kukinga mimba au waache kushiriki ngono.
Manufaa
- Hakuna madhara yanayohusishwa na dawa katika ufahamu wa uwezo wa kushika mimba. Hakuna madhara yoyote ya utumiaji, isipokuwa azinazoweza kutokea kwa kuingiza vidole ndani ya uke ili kuchunguza seviksi (kama inavyopendekezwa na baadhi ya mbinu ufahamu wa uwezo wa kushika mimba).
- Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hauna malipo au gharama ni nafuu sana. Watumiaji wanaweza kununua chati, kalenda, kipima joto cha msingi, au mifumo ya tarakilishi, au kumwajiri mkufunzi. Gharama ya moja kwa moja ni ya chini ikilinganishwa na mbinu nyingine.
- Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika pamoja na vifaa vya kuzuia mimba ili kujamiiana kuendelea katika kipindi chote ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba. Tofauti na utumiaji wa vifaa vya kuzuia mimba bila kutumia Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba, utumiaji wa ufahamu wa uwezo wa kushika mimba kunaweza kuwaruhusu wapenzi kutumia vizuia mimba wakati ambapo ni muhimu tu.
Mapungufu
- Matumizi ya zana za kizuia mimba yanahitajika katika kipindi ambapo mimba inaweza kutungwa, la sivyo lazima wanandoa waachae kushiriki ngono. Kupunguza mimba uwezekano wa kupata mimba kuwa chini ya 1% kila mwaka, kuna takriban siku 13 ambapo kushiriki ngono au vizuizi lazima vitumika wakati wa kila mzunguko mmoja.[28] Kwa wanawake wasio na mzunguko inayo badilika badilika sana - kama ilivyo kawaida wakati wa kunyonyesha, baada ya kufunga uzazi, au kama ilivyo kwa walio na magonjwa ya homoni kama vile PCOS - kuacha kujamiiana au matumizi ya vizuizi kunaweza kuhitajika katika miezi fulani. Wapenzi wengi huenda wasiwe na motisha au nidhamu ya kuacha kujamiiana au kutumia vizuizi kwa muda mrefu.
- Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hauzuii dhidi ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa.[29]
Ufaafu
Ubora wa
ufahamu ya uzazi, kama ulivyo na mbinu nyingi za kuzuia
mimba, inaweza
kutathmini kwa njia mbili. Viwango vya utumizi kamili au vya ubora wa mbinu
huzingatiwa kwa watu wanaofuata sheria zote pekee, tambua kwa usahihi kipindi
ambapo kuna uwezekano wa kutunga mimba, na uache kushiriki ngono bila kinga
katika siku ulizotambua kuwa kuna uwezekano wa kutunga mimba. Viwango vya ubora
vya matumizi halisi, au matumizi ya kawaida ni kwa
wanawake wote wanaotegemea ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ili kuzuia mimba,
ikiwa ni pamoja na wasioweza kutimiza vigezo vya "matumizi kamili".
Viwango kwa kawaida huwasilishwa katika mwaka wa kwanza wa matumizi.[30] Kwa kawaida
mfumo wa Pearl Index hutumika kukokotoa viwango vya ubora, lakini baadhi ya
tafiti hutumia majedwali ya mapunguzo.[31]
Kiwango cha
kufeli kwa ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutofautiana pakubwa kulingana na
mfumo uliotumika kubaini uwezekano wa kupata mimba, njia ya mafundisho, na
idadi ya wanaotafitiwa. Baadhi ya tafiti zimepata viwango halisi vya kufeli vya
25% kwa mwaka au zaidi.[32][33][34] Angalau
utafiti mmoja umepata kiwango cha kufeli cha chini ya 1% kwa mwaka kukiwa na
mafundisho endelevu na mapitio ya kila mwezi,[35] na tafiti
kadhaa zimegundua viwango vya kufeli halisi vya 2-3% kwa mwaka.[36][37][28][38]
Inapotumika kwa
usahihi, na kuandamana na mafundisho endelevu ya mara kwa mara, baadhi ya
tafiti zimeonyesha kuwa aina fulani za Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba huwa
na 99% ufanisi,[39][40][35][41] ulio sawa na
wa tembe za kuzuia mimba.[42]
Kutoka katika Teknolojia
ya Uzazi: [43]
- Mbinu za baada ya kudondosha yai (yaani kuacha kushiriki ngono kutoka wakati wa hedhi mpaka baada ya kudondoshwa) ina kiwango cha kufeli cha 1% kwa mwaka.
- Mbinu ya dalili na joto la mwili ina kiwango cha kufeli cha 2% kwa mwaka.
- Mbinu ya kamasi ya mlango wa kisasi pekee ina kufeli kwa kiasi cha 3% kwa mwaka.
- Mbinu ya urari wa kalenda una kiwango cha kufeli kwa 9% kwa mwaka.
- Mbinu ya Siku Wastani una kiwango cha kufeli kwa 5% kwa mwaka.
Sababu za ufanisi mdogo katika utumizi wa kawaida
Sababu kadhaa
zinachangia ufanisi wa matumizi ya kawaida kuwa ya chini zaidi kuliko ufanisi
katika matumizi kamili:
- makosa kwa upande wa watoa maelezo ya jinsi ya kutumia mbinu hii (mkufunzi kutoa taarifa isiyo sahihi au isiyokamili kuhusu mfumo wa sheria)
- makosa kwa upande wa mtumiaji (kutoelewa sheria, makosa katika kunakili)
- kutotii maelezo kimakusudi kwa watumiaji (kushiriki ngono zembe katika siku ambapo mimba inaweza kutungwa)
Sababu ya
kawaida kwa ufanisi halisi wa chini si makosa kwa upande wa wakufunnzi au
watumiaji, bali kutokana na mtumiaji kutotii sheria kimakusudi,[28][41], yaani
wanandoa kujua kwamba mwanamke anaweza kutunga mimba wakati huo, lakini
wakajihusisha katika ngono zembe bila kujali. Hii ni sawa na kufeli kwa mbinu
zuizi, ambazo kimsingi husababishwa na kutotumia mbinu hizo.
Ili kupata mimba
Kupima wakati wa kujamiiana
Utafiti uliofanywa
na Barrett na Marshall umeonyesha kuwa vitendo vya ngono visivyopangiwa huwa na
uwezekano wa 24% kutungisha mimba katika mzunguko wa hedhi. Utafiti huo pia
uligundua kuwa ngono inayolenga wakati maalumu kulingana na ufahamu unaotokana
na mbinu ya joto la kimsingi la mwili pekee ambayo ni mbinu ya Ufahamu wa Uzazi
huongeza viwango vya mimba kwa 31% -68%.
Utafiti wa
mbinu ya kamasi ya seviksi umegundua viwango vya mimba vya 67% -81% katika
mzunguko wa kwanza ikiwa kujamiiana kutatokea katika Siku ya Kilele cha ishara
za kamasi.[44][45]
Kwa sababu ya
viwango vya juu vya kutoka mimba mapema (25% ya mimba hupotea katika wiki sita
za kwanza tangu hedhi ya mwisho iliyopita ya mwanamke, au LMP), mbinu
inayotumika kuchunguza mimba inaweza kusababisha upendeleo katika viwango vya
mimba. Mbinu zilizo na uwezo wa kuonyesha mabadiliko madogo zaidi zinaweza
kuonyesha viwango vya chini vya utungaji mimba, kwa sababu huwa zinakosa
matokeo yaliyosababisha mimba kutoka mapema. Utafiti mmoja nchini Uchina kati
ya wapenzi wanaoshiriki ngono bila mpangilio ili kutungisha mimba ulitumia
mbinu ya kupima za kuchunguza mabadiliko madogo zaidi kugundua mimba. Ilipata
kiwango cha 40% cha kutungwa mimba kwa kila mzunguko katika kipindi cha utafiti
wa miezi 12.[46]
Uaguzi wa matatizo
Mizunguko ya
kawaida ya hedhi wakati mwingine huchukuliwa kuwa ushahidi kwamba mwanamke
anadondosha mayai kawaida, na mizunguko isiyo ya kawaida kuwa ushahidi kuwa
udondoshaji wa yai si wa kawaida.[47] Hata hivyo,
wanawake wengi walio na mizunguko isiyo ya kawaida hudondosha mayai kwa
kawaida, na baadhi walio na mizunguko ya kawaida kwa kweli hawadondoshi mayai
au wana matatizo katika awamu ya kutayarisha ukuta wa chupa cha uzazi. Rekodi
za joto la kimsingi la mwili, hasa, lakini pia rekodi za kamasi ya seviksi na
mkao wake, inaweza kutumika kwa usahihi kung'amua ikiwa mwanamke ana dondosha
yai, na kama urefu wa kipindi cha baada ya kudondosha yai cha mzunguko wa hedhi
inatosha kuendeleza ujauzito.
Kamasi ya
seviksi unaoweza kutunga mimba ni muhimu katika kujenga mazingira ambayo
yanaruhusu manii kupita katika mlango wa uzazi na katika viriba falopu ambako
husubiri kudondoshwa kwa yai.[48] Chati za uzazi
zinaweza kusaidia kuagua kamasi hasimu kwa uwezo wa mimba kutungishwa, sababu
ya kawaida ya kutokutungisha mimba. Ikiwa hali hii itaaguliwa, baadhi ya
washauri wanapendekeza matumizi ya guaifenesini katika siku chache kabla ya
udondoshwaji wa yai ili kupunguza uzito wa kamasi.[49]
Upiamji mimba na umri wa ujauzito
Vipimo vya
mimba si sahihi mpaka baada ya wiki 1-2 baada ya kudondoshwa yai. Kujua tarehe
inayokisiwa yai itadondoka kunaweza kumzuia mwanamke kupata matokeo yasiyo
sahihi kutokana na upimaji wa mapema mno. Pia, siku 18 mfululizo ya joto
iliyopanda, ina maanisha mwanamke ni mjamzito bila shaka.[50]
Makadirio ya
tarehe ya kudondosha yai kutoka katika chati za uzazi ni njia sahihi zaidi ya
kukadiria umri wa ujauzito zaidi ya mbinu za jadi za kupima mimba au mbinu ya
kuchunguza hedhi ya mwisho katika utaratibu wa kufuatilia hedhi.[51]
No comments:
Post a Comment